MOJA KWA MOJA: Manchester United 4-1 Leicester City

16.22pm:Na mechi inakamilika hapa Manchester United ikiibuka kidedea baada ya kuicharaza Leicester City 4-1

16.17pm: Dakika za lala salama Manchester United bado iko kifua mbele hapa dhidi ya Leicester City.

Pogba akitoa pasi murua kwa Ibrahimovic
Image caption Pogba akitoa pasi murua kwa Ibrahimovic

16.14pm: Mata anatoka Ashley Young anaingia

16.11pm: Na Rooney sasa anaingia kwa upande wa Manchester United

16.10pm: Dakika ya 82 Manchester United 4-1 Leicester City

16.09pm: Namuona Wayne Rooney akivaa jezi ishara kwamba huenda akaingia wakati wowote kutoka sasa

Wayne Rooney akijiandaa kuingia kama mchezaji wa ziada
Image caption Wayne Rooney akijiandaa kuingia kama mchezaji wa ziada

16.08pm: Carrick anaingia kwa upande wa Manchester United.

16.06pm: Leicester wanajaribu kila mbinu hapa kusawazisha lakini hali si hali kipa David De Gea anapangua mkwaju mwengine wa mfungaji wa bao la kwanza wa Leicester Gray

15.55pm: Leicester wanaamka hapa baada ya Kujipatia bao la kwanza ,na sasa wachezaji wa Man United wanalazimika kurudi nyuma ili kulinda lango lao

15.47pm: Gooooooooooal Leicester wapata bao lao la kwanza hapa kupitia mchezaji Gray baada ya kuwachenga viungo wa kati wa Man United na kupiga mkwaju ambao david De Gea hakuona kitu.

Gray akiipatia Leicester bao la kwanza hapa dhidi ya Man United
Image caption Gray akiipatia Leicester bao la kwanza hapa dhidi ya Man United

15.46pm: Leicester wamenyamazishwa hapa,na United inaendelea kutawala mechi

Kipindi cha pili kinaanza hapa kwa kasi huku Man United wakitaka kuongeza bao la tano dhidi ya mabingwa watetezi wa ligi Leicester

Na kipindi cha kwanza kinakamilika hapa Vijana wa Man United wakiwa kifua mbele.

15.12pm: Manchester United 4-0 Leicester

15.11pm: Goooooooooooal Pogba hatimaye aitikisia wavu timu yake hapa kwa mara ya kwanza baada ya kukosolewa kwa mda mrefu

Chris smalling akiiweka kifua mbele manchester United
Image caption Chris smalling akiiweka kifua mbele manchester United

15.09pm: Goaaaaaaaaaaal Manchester United wanajipatia bao ya tatu kupitia kijana Rashford hapa .Wachezaji wa Leicester wanalaumiana hapa

15.07pm: Manchester United 2-0 Leicester City

Pogba baada ya kuifungia United bao la nne Haki miliki ya picha AP
Image caption Pogba baada ya kuifungia United bao la nne

15.06pm: Gooooooooooooal ...Pogba aonana na mata vizuri hapa katika lango la Leicester kabla ya Mata kufunga bao la pili kwa niaba ya manchester United

Wayne Rooney akianza mechi ya leo miongoni mwa wachezaji wa ziada Haki miliki ya picha AP
Image caption Wayne Rooney akianza mechi ya leo miongoni mwa wachezaji wa ziada

15.02pm: Kwa kweli hawa wachezaji wa Leicester wanacheza kana kwamba tayari wamesalimu amri.kwani wamerudi nyuma na wanawacha wachezaji wa Man United kuwavamia kiholela

15.00pm: Manchester United sasa wanachukua udhibiti wa mechi hii na kusababisha hatari baada ya hatari katika lango la Leicester.

14.56pm: Manchester wanalivamia tena lango la Leicester ,Pogba achukua mpira na kumpatia pasi nzuri Ibrahimovic ,lakini anapiga mpira nje akiwa amebakia na goli.

Ibrahimovic awekwa katika uangalizi mkali hapa na nahodha wa Leicester Morgan
Image caption Ibrahimovic awekwa katika uangalizi mkali hapa na nahodha wa Leicester Morgan

14.55pm: Manchester United wavamia lango la Leicester hapa ,Ibrahimovic ampatia pasi muruwa Rashford ambaye alikuwa amebakia na kipa lakini anaupiga mpira unakuwa mwingi na unatoka lo.Rashford anakosa bao la wazi hap.

14.53pm: Manchester United 1-0 Leicester

14.52pm: Goooooooooooal Manchester United wanaongoza hapa baada ya Chris Smalling kufunga kona iliopigwa na Daley Blind.

Hakuna kupita
Image caption Hakuna kupita

14.51pm: Wanapanga mpira vizuri hawa wachezaji wa manchester United mbele ya lango la Leicester ,lakini wenye lango wanakataa.

14.49pm: Leicecter sasa wanaamka na kuanza kudhibiti mpira

14.46pm: Hatari pale katika lango la Man United baada ya kona kupigwa huku mabeki wa Mourinho wakilazimika kufanya kazi ya ziada kuwazuia washambuliaji wa Leicester.

Pogaba
Image caption Pogaba

14.45pm: Manchester United wanafanya masihara hapa na mpira unnatoka kona

14.42pm: Kikosi cha mabingwa watetezi wa ligi ya Uingereza Leicester City

Kikosi cha Leicester City
Image caption Kikosi cha Leicester City

14.40pm:Kikosi cha Manchester United

Kikosi cha Man United
Image caption Kikosi cha Man United

14.39pm: Pogba anatafuta mipira ya kumlisha Ibrahimovic lakini mabeki wa Leicester wako chonjo sana.

14.38pm: Mechi inaanza kwa mbwembwe hapa huku Manchester United ilio na wachezaji wa bei ya juu wakijaribu kuipita ngome ya Leicester

14.30pm: Manchester United vs Leicester City imeanza

Ibrahimovic akizuiliwa
Image caption Ibrahimovic akizuiliwa

Huku mabingwa wa zamani wa ligi ya Uingereza Manchester United wakikabiliana na mabingwa wa ligi msimu uliopita Leicester City, mkufunzi wa Manchester United Jose Maourinho anasema kuwa Wayne Rooney ameathiriwa na ukosoaji aliopata baada ya ushindi wa timu ya Uingereza dhidi ya Slovakia.