Man United yaiadhibu Leicester City

Paul Pogba
Image caption Paul Pogba

Klabu ya Manchester United imewacharaza mabingwa watetezi wa ligi ya Uingereza Manchester United 4-1 ,huku nahodha Wayne Rooney akichezeshwa miongoni mwa wachezaji wa ziada.

Kichwa cha Chris Smalling kiliiweka kifua mbele Man United kabla ya Juam Mata akifunga bao la pili.

Marcus Rashford na Paul Pogba -akijipatia bao lake la kwanza ,wote walifunga kupitia kona naye Demarai Gray akifunga bao zuri la kufutia machozi lililopigwa kutoka mbali kwa niaba ya Leicester.

Rooney aliingizwa kunalo dakika ya 83.