Arsenal yaicharaza Chelsea 3-0

Fabregas akimenyana na Alexis sanchez
Image caption Fabregas akimenyana na Alexis sanchez

Arsenal imepanda hadi nafasi ya tatu katika ligi ya Uingereza baada ya kucharaza Chelsea 3-0.

Alexis Sanchez alichukua fursa ya pasi mbaya iliopigwa nyuma na beki Gary Cahil katika lango la Chelsea kuiweka kifua mbele Arsenal.

Theo Walcot baadaye alifunga bao la pili baada ya Hector Bellerin kumpatia pasi nzuri ,kabla ya Mesut Ozil kufunga la tatu.

Chelsea walishindwa kujibu mchezo mzuri wa Arsenal na hawakufanikiwa kuitatiza Arsenal kutoka dakika ya kwanza hadi ya mwisho huku Batshuayi akikosa bao la wazi baada ya kusalia na Kipa alipoingia kama mchezaji wa ziada.