Michuano ya vilabu bingwa Ulaya kuendelea

Harry Kane
Image caption Harry Kane

Mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane ataendelea kuuguza jeraha lake la kifundo cha mguu wakati ambapo timu yake inakabiliana na CSKA Moscow katika kombe la vilabu bingwa Ulaya siku ya Jumanne.

Tottenham itamkosa beki wake wa kushoto Danny Rose na kiungo wa kati Eric Dier,Mousa Dembele na Moussa Sissoko.

Katika mechi nyengine itakayohusisha klabu ya Uingereza,kipa wa Leicester Kasper Schmeichel huenda akarudi kuichezea klabu yake katika mchuano wa kwanza wa kombe la vilabu bingwa Ulaya kwa klabu hiyo kushiriki nyumbani wakati watakapoikaribisha klabu ya Ureno Porto.

Schmeichel amekuwa nje kwa mechi tatu tangu Leicester iishinde Cub Brugge katika mechi yao ya ufunguzi ya Kundi G.

Mechi nyengine zitakazochezwa hii leo ni:

CSK vs Tottenham

Leicester vs FC Porto

Monaco vs Bayer Levkn

Bor Dortmd vs Real Madrid

Sporting vs Legia War

FC Copenhagen vs Club Brugge

Dinamo Zagreb vs Juventus

Sevilla vs Lyon