Wenger: Sam Allardyce anahitaji kujitetea

Mkufunzi wa Uingereza Sam Allardyce
Image caption Mkufunzi wa Uingereza Sam Allardyce

Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger amesema kuwa kocha wa Uingereza Sam Allardyce anapaswa kupewa fursa ya kujitetea dhidi ya madai katika gazeti moja.

Uchunguzi wa gazeti la Daily Telegraph unasema kuwa Allardyce mwenye umri wa miaka 61,alitumia cheo chake kushauriana mpango wa pauni 400,000 na kutoa ushauri kuhusu vile anaweza ''kuzunguka'' sheria za uhamiaji wa wachezaji.

Mkufunzi huyo wa zamani wa timu ya Bolton,Newcastle na West Ham pia amelikosoa shirikisho la soka nchini Uingereza FA, aliyemrithi Roy Hodgson, na aliyekuwa naibu wake Gary Neville.

''Ni muhimu kumwacha Allardyce kujitetea na ninatumai atasafisha jina lake'',alisema Wenger.

Allardyce bado hajajibu madai hayo,na amekuwa akikutana na mwenyekiti wa FA Greg Clarke na afisa mkuu wa shirikisho hilo Martin Glenn Jumanne.