Europa League: Manchester United kukabiliana na Zorya Luhansk

Manchester United Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Manchester United wako nafasi ya mwisho katika ligi ya yuropa baada ya kupoteza katika mechi ya ufunguzi dhidi ya Feyenoord

Kukutana na klabu ya Manchester United katika uwanja wa Old Trafford katika ligi ndogo ya klabu bingwa Ulaya, Europa League, siku ya Alhamisi itakuwa ya 'kuogofya' amesema meneja Yuriy Vernydub wa klabu ya Zorya Luhansk ya Ukraine.

Mechi hiyo itaanza saa nne na dakika tano usiku Afrika Mashariki.

Klabu hiyo ya Zorya Luhansk, ilimaliza katika nafasi ya nne katika ligi ya Ukraine msimu uliopita na wanaanza mechi yao ya kwanza katika hatua ya makundi.

''Hakuna sababu ya kujiepusha. Tunaelewa kwamba Manchester United ni klabu ya kimataifa,'' amesema Vernydub.

Nahodha wa United Wayne Rooney alikuwa anatarajiwa kujiunga katika kikosi cha kwanza cha watu kumi na moja lakini amekuwa na shida ya mgongo.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wayne Rooney

Mshambuliaji huyo,30, aliachwa nje katika mechi iliyochezwa wikendi iliyopita katika ligi ya premia waliyoondoka na ushindi dhidi ya Leicester City.

Meneja Jose Mourinho amesema: ''Nilikuwa nimeamini kumchezesha kutoka mwanzo (siku ya Alhamisi) lakini kwa jinsi mambo yalivyo hivi karibuni sina uhakika.''

Mourinho amethibitisha mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic, ataanza katika wachezaji 11 wa kwanza, lakini mashetani hao wekundu watamkosa kiungo wa kati Henrikh Mkhitaryan, huku Luke Shaw akiwa hajulikani hali yake baada ya kurudishwa nyumbani siku ya Jumatano kutokana na maradhi.

Mechi nyingine zitakazochezwa leo

 • Fenerbahçe v Feyenoord - Ulker Stadyumu
 • Machester Utd v Zorya Luhansk - Old Trafford
 • Fiorentina v FK Qarabag- Artemio Franchi
 • Slovan Liberec v PAOK Salonika- U Nisy
 • Hapoel Be'er Sheva dhidi ya Southampton-Yaakov Turner Toto Stadium
 • Sparta Prague v Inter Milan-Generali Arena
 • FC Zürich v Osmanlispor -Letzigrund Stadion
 • Steaua Buc v Villarreal-National Arena
 • FC Astana v BSC Young Boys-Astana Arena
 • Olympiakos v Apoel Nic- Georgios Karaiskakis Stadium
 • FK Qabala v 1. FSV Mainz 05- Bakcell Arena
 • Saint-Étienne v Anderlecht-Stade Geoffroy-Guichard
 • Dundalk v M'bi Tel-Aviv- Tallaght Stadium
 • Zenit St P v AZ Alkmaar-Petrovski Stadium
 • FK Austria Vienna v Viktoria Plzen-Ernst-Happel-Stadion
 • Roma v Astra Giurgiu-Olimpico
 • Ath Bilbao v Rapid Vienna-San Mamés
 • KRC Genk v Sassuolo- Cristal Arena
 • Ajax v Standard Liege- Amsterdam ArenA
 • Celta Vigo v Panathinaikos- Balaídos
 • KAA Gent v Konyaspor- Ghelamco Arena
 • Shakt Donsk v Sporting Braga- Arena Lviv
 • Schalke v FC RB Salzb- VELTINS-Arena
 • FK Krasnodar v Nice -Kuban Stadium