Liverpool yawashinda Swansea mabao 2-1

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption James Milner ameifungia Liverpool mabao manne msimu huu

Penalti ya dakika za misho ya James Milner iliwapa Liverpool ushindi dhdi wa Sansea na kumuongezea na kumuongezea matatizo kocha wa Swansea Francesco Guidolin.

Swansea ilipata bao la kwanza kupitia kwa Leroy Fer.

Hata hivyo Roberto Firmino alisawazisha muda mfupi baada ya kuanza kwa kipindi cha pili kutokana na pasi aliyopata kutoka kwa Jordan Henderson.

Milner aliifungua Liverpool bao la ushindi dakika sita kabla ya mechi kumalizika kwa njia ya penalti baada ya Firmino kufanyiwa madhambi.

Bao hilo lilikuwa ni zawadi kwa Liverpool ambao waliitawala mechi katika kipindi cha pili.