Man United yashindwa kutamba dhidi ya Stoke

Man United yashindwa kutamba dhidi ya Stoke City nyumbani Old Trafford
Image caption Man United yashindwa kutamba dhidi ya Stoke City nyumbani Old Trafford

Klabu ya Stoke City ilijipatia pointi moja katika uwanja wa Old Trafford baada ya Joe Allen kusawazisha na hivyobasi kuiadhibu Manchester United iliotawala mechi hiyo kwa kipindi cha mda mrefu.

Baada ya kipa wa Stoke kuokoa mashambulio mengi katika kipindi cha kwanza cha mechi,United ilijiweka kifua mbele baada ya mchezaji wa ziada Anthony Martial kufunga bao la kwanza.

Ilikuwa pigo kubwa kwa Stoke ambayo ilikuwa haijafanya shambulio lolote katika ngome ya United.

Lakini baada ya Jon Walters kupiga krosi, Allen alifika na kusawazisha hivyobasi kufuinga midomo ya mashabiki wa United ambao walikuwa wakiimba katika kipindi chote cha mchuano huo.

Stoke City ambayo iko katika nafasi ya pili kutoka mwisho sasa imejiongezea matumaini ya kuondoka katika eneo la mkia la ligi hiyo ya Uingereza.