Manchester City yalazwa na Tottenham

Dele Ali akiifungia Manchester City bao la pili
Image caption Dele Ali akiifungia Manchester City bao la pili

Klabu ya Whitehart Lane nchini Uingereza Tottenham Hotspurs iliisitisha rekodi ya Manchester City ya kutofungwa.

Goli la kujifunga wenyewe la Aleksander Kolarov liliiweka Tottenham kifua mbele baada ya kuichanganya krosi ya Danny Rose alipokuwa akijaribu kuokoa na hivyobasi mpira kumpita kipa Claudio Bravo.

Dele Ali aliongeza bao la pili ndani ya eneo hatari la City kufuatia pasi nzuri ya Son Heung-min.

Spurs walipata penalti wakati Ali Dele alipoangushwa na Fernandinho katika lango la Manchester City,lakini Bravo aliokoa mkwaju wa Erik Lamela.