Arsenal yailaza Burnley

Arsenal yailaza Burnley
Image caption Arsenal yailaza Burnley

Burnley ilishindwa kulinda lango lake katika dakika za mwisho za mechi dhidi ya Arsenal na kuwawacha wageni hao wa Emirates kupata ushindi wa bao moja lililofungwa na beki Koscielny.

Katika dakika za ziada,Theo Walcot alipata pasi nzuri kutoka kwa Oxlaide Chamberlain ambaye kichwa chake kilienda karibu na Kolscieny ambaye alikuwa amesimama katika lango la Burnley.

Burnley walipata fursa kadhaa ,wakati Sam Voks alipopiga juu akiwa amesalia na goli huku kichwa cha Michael Keane kikipga chuma cha goli.

Lakini licha ya Burnley kuwazuia Arsenal kwa kipindi kirefu cha mechi ,hatimaye walifunguka katika dakika za mwisho za mechi na kuruhusu bao hilo la Koscielny.