Eto'o arejeshwa katika kikosi cha timu ya Antalyaspor

Samuel Eto'o alijiunga na klabu ya Antalyaspor June 2015
Image caption Samuel Eto'o alijiunga na klabu ya Antalyaspor June 2015

Klabu ya soka ya Antalyaspor ya Uturuki imemjumuisha kikosini mshambuliaji wake Samuel Eto'o katika mchezo unafouata dhidi ya Galatasaray hii ikiwa ni kinyume na matarajio ya wengi.

Mwenyekiti wa Antalyaspor Ali Safak Ozturk amesema kuwa Eto'o ameomba radhi na mwenye moyo mgumu mithili ya jiwe linalokaa majini na haliingii maji ndio tu anapaswa kutokumsahe.

''Tunatumai atajirekebisha na atakuwa na mchango mkubwa katika timu yetu''Ozturk amekiambia kikosi cha timu hiyo.

Hivi karibuni mshambuliaji huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Cameroon aliwekwa nje ya kikosi hicho kutokana na kutoa maneno ya kibaguzi kwa uongozi wa klabu hiyo aliyoyaweka katika mtandao wake wa Instagram akisema kuwa ''yamkini baadhi ya watu hawaniheshimu kwa sababu mimi ni mweusi''