Iwobi na Iheanacho waifungia Nigeria

Mchezaji wa Arsenal Alexi Iwobi alishiriki katika mechi ya Nigeria dhidi ya Zambia
Image caption Mchezaji wa Arsenal Alexi Iwobi alishiriki katika mechi ya Nigeria dhidi ya Zambia

Nyota wa Nigeria wameingia katika mitandao ya kijamii kusherehekea ushindi wao wa kwanza katika harakati za kufuzu katika kombe la dunia la mwaka 2018.

''The Super Eagles'' kama wanavyojiita walipata ushindi wa ugenini wa 2-1 dhidi ya Zambia siku ya Jumapili katika kundi B,katika mechi yao a kwanza ya kufuzu kwa kombe la dunia.

Mabao ya Nigeria yalifungwa katiika kipindi cha kwanza na wachezaji wawili wa ligi ya Uingereza.

Image caption Wachezaji wa Nigeria katika mtandao wa Twitter wakisheherekea ushindi wao dhidi ya Zambia

Mchezaji wa Arsenal Alex Iwobi alikuwa wa kwanza kuifungia Nigeria katika dakika ya 32,kabla ya mshambuliaji Iheanacho Kelechi wa Manchester City kuongeza bao la pili dakika 10 baadaye.

Nigeria sasa inaongoza kundi hilo ,baada ya Algeria kupata sare ya 1-1 dhidi ya Cameroon katika kundi hilo.

Kwengineko,Misri iliishinda Congo 2-1 mjini Brazzaville katika kundi E na katika kundi A Tunisia iliishinda 2-0 dhidi ya Guinea.