Argentina watandikwa Peru mechi ya kufuzu Kombe la Dunia

Lionel Messi Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Argentina walikuwa bila Lionel Messi ambaye majuzi alibadilisha uamuzi wake wa kustaafu soka ya kimataifa

Mechi za Raundi ya 10 ya nchi za kanda ya Marekani ya Kusini chini ya Mwamvuli wa Shirikisho lao CONMEBOL kusaka nchi 4 zitakazotinga moja kwa moja huko Urusi Mwaka 2018 kwenye Fainali za Kombe la Dunia zimeendelea alfajiri hii na Vinara Uruguay kushushwa toka kileleni na Brazil wakati Argentina ikitandikwa nyumbani kwao.

Wakicheza Ugenini huko Estadio Olímpico Metropolitano de Mérida, Mérida, Brazil waliwafunga wenyeji Venezuela 2-0 kwenye Mechi iliyosimama kwa dakika 10 kuanzia Dakika ya 75 baada ya taa za Uwanjani kuzimika.

Mabao ya Brazil, waliocheza bila nahodha wao Neymar anayetumikia marufuku ya mechi moja, yalifungwa na Gabriel Jesus, dakika ya 8, na Willian, dakika ya 53.

Nao Uruguay walitoka sare 2-2 na Colombia kwenye mechi iliyochezwa huko Uruguaya huku mabao ya wenyeji yakifungwa dakika za 27 na 73 na Rodriguez na Luis Suarez huku za Colombia wakifunga dakika ya 15 na 84 kupitia Aguilar na Mina.

Argentina wakicheza ugenini huko Lima, Peru bila nyota wao Lionel Messi walifungwa 1-0, bao lililopatikana dakika ya 18 kupitia Derlis González.

Baada ya Mechi 10 kwa kila timu, Brazil ndio wanaongoza wakiwa na alama 21 wakifuata Uruguay alama wenye 20, kisha Ecuador na Colombia zikiwa na alama 17 kila mmoja na Argentina ni wa 5 wakiwa na alama 16.