Stan Wawrinka ang’ara dhidi ya Kyle Edmund

Kyle Edmund Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kyle Edmund ameorodheshwa nambari 48 duniani

Mwingereza Kyle Edmund ametolewa katika mashindano ya tenisi ya Shanghai Master katika raundi ya pili ya michuano hiyo baada ya kufungwa na Stan Wawrinka.

Alishindwa kwa seti mbili 6-3 na 6-4 baada ya kupoteza mechi tano.

Huu ni ushindi wa tatu wa Wawrinka na amesema anajisikia mwenye furaha sana kwa kushinda mchezo huo kwa kuwa alikuwa hatarajii kucheza vizuri.

Katika mchezo ujao Wawrinka huenda atakutana na Mfaransa Gilles Simon au Wu Di kutoka China.

Edmund wiki hii alipanda katika viwango vya ubora kwa kufikia namba 48.