Serge Aurier aokoa maisha ya mchezaji wa Mali

Serge Aurier Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Aurier (kati) alichukua hatua upesi kumsaidia Doumbia (namba 12, kulia).

Beki wa klabu ya Paris Saint-Germain kutoka Ivory Coast Serge Aurier amesifiwa sana baada yake "kuokoa maisha" ya mchezaji wa Mali Moussa Doumbia Jumamosi

Doumbia alianguka na kupoteza fahamu baada ya kukabwa na Lamine Kone wa Sunderland.

Aurier aliingia kati baada ya kuona mchezaji huyo wa Rostov alikuwa anakaribia akamlaza kwa upande na kumzuia kuumeza ulimi wake.

Meneja wa Mali Alain Giresse amesema alizungumza na Aurier baada ya mchezo huo na kumshukuru.

"Wachezaji wote waligundua kwamba Doumbia alikuwa anakabwa kooni na kushindwa kupumua na alikuwa karibu kuumeza ulimi wake," Giresse, redio ya Ufaransa ya RMC.

"Ni hapo ambapo Aurier, akiwa na mmoja wa wachezaji wetu, alichukua hatua haraka wakamlaza upande na kuutoa ulimi wake, kwa sababu alikuwa anakaribia kupoteza maisha."

Ivory Coast walishinda 3-1 mechi hiyo ya kufuzu kwa Kombe la Dunia 2018.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii

Kuhusu BBC

Mitandao inayohusiana

BBC haina haihusiki vyovyote na taarifa za mitandao ya kujitegemea