Kocha wa Uingereza asema kikosi chake ni kibovu

Kocha wa Uingereza Gareth Southgate kushoto
Image caption Kocha wa Uingereza Gareth Southgate kushoto

Kocha wa muda wa timu ya taifa ya Uingereza, Gareth Southgate amesema alirithi kikosi kibovu baada ya kutoka sare ya bila kufungana na Slovenia katika mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia jana.

Southgate alichukua mikoba ya Sam Allardyce mwezi uliopita kwa ajili ya kuisimamia timu hiyo katika mechi zake nne ambapo mpaka sasa ameshinda mchezo mmoja dhidi ya Malta kabla ya sare ya jana waliyopata.

Uingereza ambao wanaongoza kundi F, walipata alama hiyo moja jana kufuatia juhudi za hali za juu zilizoonyeshwa na kipa wake Joe Hart.

Southgate amesema wakati alipoichukua timu haikuwa sawa lakini taratibu anaona kama kikosi hicho kinaimarika.