Arsenal washinda, Man City sare na Everton

Theo Walcott Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Theo Walcott amefunga mabao matano katika mechi nane alizocheza msimu huu

Mabingwa watetezi wa Lig ya Premia Leicester City wamecharazwa 3-0 na Chelsea uwanjani Stamford Bridge nao Arsenal wakafanikiwa kuondoka na ushindi dhidi ya Swansea City licha ya kusalia na wachezaji 10 uwanjani.

Mabao ya Chelsea yalifungwa na Diego Costa, Eden Hazard na Victor Moses.

Theo Walcott alifunga mawili upande wa Arsenal kabla ya Gylfi Sigurdsson kukomboa moja upande wa Swansea.

Mesut Ozil aliwarejesha Arsenal mabao mawili mbele baada ya kufikia krosi ya kabla ya nguvu mpya Borja Baston kufunga la pili upande wa Swansea.

Granit Xhaka wa Arsenal alioneshwa kadi nyekundu lakini wakafanikiwa kukwamilia ushindi wao.

Uwanjani Etihad, vijana wa Pep Guardiola wametoka sare 1-1 na Everton. Everton walitangulia kufunga kupitia Romelu Lukaku. City walikomboa kupitia Nolito.

Mechi iliyoshangaza wengi ni ya Bournemouth ambao wamepata ushindi mkubwa wa 6-1 dhidi ya Hull City.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Maarten Stekelenburg wa Everton aliokoa mikwaju miwili ya penalti

Matokeo kamili ya mechi za leo

  • Arsenal 3-2 Swansea
  • Bournemouth 6-1 Hull
  • Man City 1-1 Everton
  • Stoke 2-0 Sunderland
  • West Brom 1-1 Tottenham
  • Chelsea 3-0 Arsenal