Mashindano ya mbio za magari Rwanda

Mbio za magari
Image caption Washiriki ni kutoka Rwanda, Burundi, Uganda na Kenya

Mashindano ya kimataifa ya mbio za magari yameanza leo katika mji wa Huye kusini mwa Rwanda.

Washiriki ni kutoka nchi za afrika mashariki Rwanda, Burundi, Uganda na Kenya.

Jumamosi hii magari yanazunguka maeneo kadhaa ya nje ya mji wa Huye, umbali wa kilomita 151 ambao usiku pia watazunguka umbali wa km 300.

Dereva anayeogopwa sana katika mashindano haya ni msichana kutoka Uganda, Leila Mayanja Blick anayeendesha gari aina ya Toyota Runx.