Guardiola: Barcelona ni ''mashine''

Mkufunzi wa manchester City Pep Guardiola alipokuwa akiifunza Barcelona Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mkufunzi wa manchester City Pep Guardiola alipokuwa akiifunza Barcelona

Barcelona ni ''mashine'' ambayo huenda ikatawala mechi dhidi ya Manchester City siku ya jumatano ,kulingana na Pep Guardiola.raia huyo wa Uhispania alishinda kombe la Ulaya akiwa mchezaji na kocha wakati alipokuwa akiiongoza timu hiyo la La Liga.

Ataelekea tena Nou Camp katika mechi ya vilabu bingwa Ulaya wiki ijayo akijua kibarua kigumu kinachoisubiri timu yake.

''Barcelona ni timu maalum kutokana na mchezo wao,Ni mashine'',alisema.

Image caption Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola

''Itachukua muda mrefu kuweza kufikia kiwango cha Barcelona,Muongo mmoja uliopita,miaka 50 iliopita Barcelona imekuwa ikitawala katika soka'' .

''Napenda wanavyocheza'',aliongezea.''Wana wachezaji watatu wazuri sana -lionel Messi,Luis Suarez na Neymar mbele.ni washambuliaji hatari.Wana timu nzuri''.