Refa wa mechi kati ya Man United na Liverpool atiliwa shaka

Refa Taylor anadaiwa kuwa mkazi wa Manchester hivyobasi wengi wanahisi atapendelea mechi hiyo Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Refa Taylor anadaiwa kuwa mkazi wa Manchester hivyobasi wengi wanahisi atapendelea mechi hiyo

Mkufunzi wa klabu ya Manchester United anasema kuwa refa Anthony Taylor atakabiliwa na wakati mgumu wakati atakaposimamia mechi ya klabu yake dhidi ya Liverpool.

Taylor anayetoka eneo la Manchester alikosolewa na Keith Hackett, kiongozi wa zamani wa wasimamizi wa mechi.

Uamuzi huo pia umetiliwa shaka na mashabiki wa Liverpool katika mitandao ya kijamii.

Mourinho anasema kuwa mtu mwenye malengo maovu anampiga presha Taylor anayeungu mkono timu ya Altrincham ambayo haiko katika ligi ya EPL.

Swala kama hilo msimu uliopita lilisababisha kuondolewa kwa refa anayetoka Leicester Kevin Friend katika mechi ya Tottenham huko Stoke baada ya Spurs na Leicester kuwa katika wakati muhimu wa kushinda ligi.

Mourinho aliyemrithi Louis Van Gaal amesema kuwa refa Taylor ni mzuri sana.

Hatahivyo raia huyo wa Ureno amesema kuwa : Nahisi itakuwa vigumu kwake kuchezesha mchezo mzuri.