Joshua na Klitschko wakubaliana kuzipiga

Bondia wa uzani mzitokutoka Uingereza Anthony Joshua kuzipiga na Wladmir Klitschko kutoka Ukraine Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Bondia wa uzani mzitokutoka Uingereza Anthony Joshua kuzipiga na Wladmir Klitschko kutoka Ukraine

Bondia wa Uingereza Anthony Joshua na bondia wa Ukraine Wladmir Klitschko wamekubali kupigana huku tangazo la pigano hilo likitarajiwa kufanywa katika siku chache zijazo,kulingana na promota Eddie Hearn.

Kulingana na Hearn,pigano hilo la uzani mzito linafaa kuidhinishwa na ukanda wa Joshua wa IBF mbali na mikanda ya WBA na WBO.

Siku ya Jumatano bingwa wa ndondi katika uzani mzito duniani Tyson Fury alisalimu mataji yake ya WBO na WBA huku leseni yake ya kupigana ikifutiliwa mbali kwa muda.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Anthony Joshua wa Uingereza anashikilia taji la IBF duniani

Bodi ya Uingereza inayodhibiti leseni za mabondia ilimpokonya bondia huyo leseni yake kufuatia uchunguzi wa kutumia dawa za kusisimua misuli,baada ya bondia huyo mwenye umri wa miaka 28 kukiri kwamba amekuwa akitumia Cocaine ili kukabiliana na msongo wa mawazo.