Mourinho kuchunguzwa na FA juu ya kauli kwa mwamuzi

Mourinho amesema itakuwa vigumu kwa mwamuzi huyo kuchezesha vizuri baada ya uteuzi wake kukosolewa.
Image caption Mourinho amesema itakuwa vigumu kwa mwamuzi huyo kuchezesha vizuri baada ya uteuzi wake kukosolewa.

Matamshi ya Jose Mourinho kuhusu uteuzi wa mwamuzi anaeshabikia Manchester United Anthony Taylor kwa mchezo wa ligi kuu England kati ya Manchester United dhidi ya Liverpool utakaochezwa leo jumatatu yatachunguzwa na Shirikisho la Mpira wa miguu nchini humo FA.

Mourinho amesema itakuwa vigumu kwa mwamuzi huyo kuchezesha vizuri baada ya uteuzi wake kukosolewa.

'Mtu mmoja akiwa na lengo anaweka shinikizo kwake' alisema Mourinho

Kwa kawaida makocha hawatakiwi kuzungumza lolote kuhusiana na mwamuzi kabla ya mchezo.

Image caption Anthony Taylor hajatoa kadi yoyote nyekundu msimu huu

FA inataka kuchunguza matamshi hayo kabla ya kuamua ni hatua gani kama ipo inaweza kuchukuliwa.

Uteuzi wa Taylor, umekosolewa na Kenith Hackett,mkuu wa Bodi ya marefarii Professional Game Match Officials Ltd