Tennis: Kyrgios afungiwa kucheza wiki nane

Nick Kyrgios
Image caption Nick Kyrgios

Muaustralia Nick Kyrgios amefungiwa kwa wiki nane na kutozwa faini ya dola za kimarekani 25,000 kwa utovu wa nidhamu-ikiwa ni pamoja na kucheza ovyo wiki iliyopita michuano ya Shaghai Masters.

Nick mwenye miaka 21 amekuwa akigongesha mpira juu ya wavu mara kadhaa katika mchezo aliofungwa Mischa Zverev kwa seti 6-3 6-1 .

Mchezaji huyo nambari 14 kwa ubora duniani ameomba radhi kwa tukio hilo na kusema atafanyia kazi wakati huu akiwa kifungoni.

Wiki iliyopita Muingereza Andy Murray alisema hafikirii kuwa faini pekee itakuwa adhabu tosha.

Mwaka 2015 Kyrgios alifungiwa siku 28 na faini ya dola 25,000 baada ya kutoa maneno ya kashfa kwa mpenzi wa Stan Wawrinka katika michuano ya kombe la Rogers.