Mourinho: Tulidhibiti mechi na kuwanyamazisha mashabiki wao

Mkufunzi wa man United Jose Mourinho
Image caption Mkufunzi wa man United Jose Mourinho

Mkufunzi wa klabu ya Manchester United Jose Mourinho amesema kuwa timu yake ilidhibiti mpira pamoja na kufunga midomo ya mashabiki wa Anfield.

Akihojiwa baada ya mechi hiyo iliotoka sare ya bila kwa bila,Mourinho amesema kuwa ijapokuwa hakutarajia matokeo hayo timu yake ilifanikiwa kuizuia Liverpool kwa kudhibiti mchezo kwa muda mrefu.

''Tulifanikiwa kudhibiti kelele za mashabiki wa Anfield pamoja na mchezo wa timu yao''.

Mourinho amesema kuwa ijapokuwa wengi walidhani watashindwa timu yake iliodhibiti mpira na kuwapatia kibarua kigumu wapinzani wao.

Hatahivyo mkufunzi huyo amekiri kwamba safu ya ushambuliaji ya Manchester United haikuwa imara wakati wa mechi hiyo.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Man United ikichuana na Liverpool katika uga wa Anfield .Mechi hiyo ilikamilika katika sare ya bila kwa bila

''Hatahivyo nadhani hatukuimarika vilivyo katika safu ya mbele.Nashukuru kwamba pointi yetu moja iliwazuia kupata tatu''.

Aliongezea kwamba timu yake ina kibarua kigumu katika uwanja wa Stamford bridge wikendi ijayo na hivyobasi watalazimika kuimarika.

Katika mechi hiyo Liverpool lifanikiwa kudhibiti mechi kwa asilimia 65 huku Manchester United ikidhibiti asilimia 35.