Leicester City yang'ara UEFA

Riyad Mahrez na Islam Slimani waling'ara katika mchezo huo
Image caption Riyad Mahrez na Islam Slimani waling'ara katika mchezo huo

Klabu ya soka ya Leicester City imeendeleza wimbi la ushindi katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya FC Copenhagen.

Wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani King Power, Leicester walipata bao hilo dakika tano kabla ya kwenda mapumzikoni kupitia kwa Riyad Mahrez aliyekuwa katika kiwango cha hali ya juu baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Mualgeria mwenzake Islam Slimani.

Image caption Islam Slimani alikataliwa bao baada ya kuotea

Kwa matokeo hayo Leicester wanabaki kileleni mwa kundi G wakiwa na alama 9 baada ya kushinda michezo yote mitatu ya ufnguzi wa ligi ya mabingwa Ulaya.

Timu pekee zilizowahi kushinda michezo mitatu ya ufunguzi katika michuano hiyo ni AC Milan, Paris St-Germain, Juventus na Malaga.

Matokeo mengine ya Ligi ya mabingwa barani Ulaya

Bayer 04 Leverkusen 0-0 Tottenham Hotspur F.C.

CSKA Moscow 1-1 AS Monaco FC

Real Madrid 5-1 Legia Warsaw

Sporting 1 -2 Borussia Dortmund

Club Brugge 1-2 FC Porto

Dinamo Zagreb 0- 1 Sevilla

Lyon 0- 1 Juventus