Wenger: Nisingeweza kumuuza Walcott

Mshambuliaji wa Arsenal Theo Walcott akiwa na mkufunzi Arsene Wenger
Image caption Mshambuliaji wa Arsenal Theo Walcott akiwa na mkufunzi Arsene Wenger

Mkufunzi wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger anasema kuwa hakuwahi kufikiria kwamba angemuuza mshambuliaji wa Uingereza Theo Walcot msimu uliopita.

Walcott alianza mechi 15 za ligi ya Uingereza msimu uliopita,na kuweza kufunga mabao 5, jumla ambayo ameweza kuifikia katika mechi nane alizocheza msimu huu.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 anatarajiwa kuanza katika mchuano wa kombe la vilabu bingwa dhidi ya Ludogorets Razgaard siku ya Jumatano.

''Sikuwa tayari kumuachilia.Kila mara nilitaka aendelea kuwa nasi'',alisema Wenger.

''Nimehisi hivyo tangu aanze kucheza na uhuru mwingi,pengine amekuwa akicheza na hisia na hapigi mahesabu ya iwapo nifanye hili ama nifanye lile''?

''Nadhani hana mtazamo wenye vikwazo vingi na hilo linaonyesha kwamba ni mchezaji tofauti sana''.

Arsenal wanakabiliana na wapinzani wao wa Bulgaria wakijua kwamba ushindi mara mbili utaipatia fursa ya kusonga mbele katika michuano ya vilabu bingwa Ulaya.

Walitoka sare na PSG ya Ufaransa kabla ya kuishinda Basel 2-0