Dulla Mbabe kupigana na Mchina Dar

Bango la pambano Haki miliki ya picha Other

Bondia wa Tanzania Dulla Mbabe anatarajia kupambana na Bondia Chengbo Zheng kutoka Taifa la China tarehe 28 Oktoba, Pambano la WBO katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.

Kwa mujibu wa mwandaaji wa pambano hilo Jay Msangi, mshindi wa pambano hilo atajinyakulia Mkanda wa ubingwa, huku pia kukiwa na mapambano mengine mengi ya utangulizi ambayo yatawakutanisha mabondia kutoka Tanzania na nje ya Tanzania.

Jay Msangi amesema kwa sasa wataandaa mapambano mengi ya kimataifa kwa mabondia wa Tanzania kwa lengo la kuwandaa kufuzu mashindano ya Olimpiki nchini Japan.