Afcon 2017: Ivory Coast uso kwa uso na kocha wake wa zamani Herve Renard

Morocco and Ivory Coast watachuana mara tatu ndani ya miezi michache ijayo
Image caption Morocco and Ivory Coast watachuana mara tatu ndani ya miezi michache ijayo

Timu ya taifa ya Ivory Coast itapambana na kocha wake wa zamani Herve Renard baada ya kupangiwa katika kundi moja na Morocco katika michuano ya fainali za kombe la mataifa ya Afrika.

Renard aliiongoza Ivory Coast katika fainali za kombe hilo mwaka 2015 na sasa anakwenda tena Gabon akiwa na kikosi cha nchi tofauti.

Gabon watafungua mashindano hayo Januari 14, huku mchezo wa fainali ukipangwa kuwa Februari 5.

Muonekano wa timu na makundi AFCON 2017

KUNDI A

Gabon

Burkina Faso

Cameroon

Guinea Bissau

KUNDI B

Algeria

Tunisia

Senegal

Zimbabwe

KUNDI C

Ivory Coast

DR Kongo

Morocco

Togo

GROUP D

Ghana

Mali

Misri

Uganda