Pep Guardiola: Sitobadili filosofia ya mchezo wangu

Mkufunzi wa Chelsea Pep Guardiola
Image caption Mkufunzi wa Chelsea Pep Guardiola

Meneja wa Manchester City Pepe Guardiola anasema kuwa hatobadili filisofia yake licha ya klabu yake kufungwa 4-0 na Barcelona katika uwanja wa Nou camp.

Lionel Messi alifunga hat-trick dhidi ya Manchester City iliokuwa na safu ya ulinzi ilio legea huku kipa Claudio Bravo akipewa kadi nyekundu kwa kushika mpira nje ya eneo hatari.hakutakuwa na mabadiliko.

''Hadi siku ya mwisho ya kazi yangu kama mkufunzi nitajaribu kucheza kwa uwezo wetu'',alisema.

Barcelona inaongoza kundi C na pointi tisa ,ikiwa mbele kwa pointi tano.

City ilikuwa nyuma kwa bao moja katika dakika za kwanza za kipindi cha pili wakati Bravo aliposhika mpira na bahati mbaya ukamuangukia Luis Suarez.