Mourinho: Pogba apewe muda Man Utd

Paul Pogba Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Paul Pogba aliondolewa uwanjani dakika ya 75 Alhamisi dhidi ya Fenerbahce

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amesema hakutarajia Paul Pogba, ambaye alicheza vyema sana dhidi ya Fenerbahce katika ligi ndogo ya Ulaya, azoee soka ya England haraka.

Amesema mchezaji huyo anafaa kupewa muda kuzoea kucheza tena England badala ya kukosolewa kila mara.

Pogba, 23, aliyenunuliwa £89m mwezi Agosti na kuvunja rekodi ya dunia, alifunga mabao mawili Alhamisi wakati wa ushindi wao wa 4-1 dhidi ya Fernabahce.

Hata hivyo hakung'aa Jumatatu dhidi ya Liverpool mechi waliyotoka sare 0-0.

"SIku mbili zilizopita, alitajwa kuwa mchezaji mbaya zaidi katika Lgi ya Premia na saa 48 anasifiwa sana," amesema Mourinho.

"Anahitaji muda. Naridhishwa na uchezaji wake. Ana ustadi tunaohitaji."

Mourinho amesema anaamini Pogba bado anazoa aina tofauti ya soka.

"Niliwa Italia na nafahamu sifa za soka huko, kasi yake na ukali wake," Mourinho, 53, alisema.

"Kuwa Italia kwa miaka minne au mitano na kisha urejee Ligi ya Premia, sikumtarajia aanze mara moja kung'aa."

Haki miliki ya picha @PaulPogba
Image caption Ujumbe wa Pogba kwenye Twitter

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii