Marcello Lippi kuifunza timu ya taifa China

Marcello Lippi Haki miliki ya picha Getty Images

Marcello Lippi - aliyeshinda kombe la dunia mnamo mwaka 2006 na timu ya taifa ya Italia - amerudi katika soka baadaya kustaafau na sasa ndiye mkufunzi wa timu ya China.

Lippi, mwenye umri wa miaka 68, alisimamia timu ya Italia mara mbili na kushinda matajai matano ya Serie A na taji la ubingwa barani Ulaya na timu ya Juventus.

Alistaafu ukufunzi baada ya kushinda taji la tatu mtawalai la ligi na timu ya Uchina Guangzhou Evergrande mnamo 2014.

China imeorodheshwa katika nafasi ya 84 duniani.

Sasa anaichukua nafasi ya Gao Hongbo, aliyejiuzulu mapema mwezi huu baada ya kuishinda Uzbekistan 2- 0 jambo linalodidimiza matumaini ya China kufuzu kwa kombe la dunia 2018 nchini Urusi.