Bournemouth 0 - 0 Tottenham

Bournemouth v Tottenham Haki miliki ya picha Getty Images

Tottenham imekosa nafasi ya kusogea juu katika orodha ya Premier League - angalau kwa saa kadhaa - baada ya kuzuiwa kwa sare ya 0-0 kwa wenyeji Bournemouth.

Bournemouth nusra wachukuwe uongozi wa mapema wakati Charlie Daniels aliposukuma tobwe lililookolewa na Hugo Lloris, Kipa huyo wa Spurs alifanikiwa kuuzuia mpira na miguu yake.

Licha ya kuwa wageni Spurs walijiimarisha katika nusu ya pili ya echi wenyeji walikaba mchezo, huku kipa Artur Boruc akimzuia Dele Alli na Danny Rose, wakati Benik Afobe wa Bournemouth alipoingia uwanjani karibu kipindi cha mwisho.

Wakati huo huo refa Craig Pawson aliwauadhi mashambiki wa nyumbani waliohisi Lamela angepaswa kuonyeshwa kadi ya njano ya pili, huku naye Moussa Sissoko hakuadhibiwa kwa kumdunga kisuku suku usoni Harry Arter.

Pawson baadaye alikataa ombi la dakika ya mwisho la Bournemouth kutaka penalti wakati Jack Wilshere alipoanguka baada ya kuchengwa na Jan Vertonghen.

Makocha wote wamesifia umahiri wa timu pinzani kuelekea kuanza mechi hiyo na haikushangaza mchezo ulivyoanza kwa kasi kubwa na pande zote zikishambulia upande mpinzani kwa urahisi.