Mourinho: Sitosherehekea kama ''mtoto mwenye wazimu''

Mourinho akisherehekea ushindi wa Chelsea alipokuwa mkufunzi wa klabu hiyo
Image caption Mourinho akisherehekea ushindi wa Chelsea alipokuwa mkufunzi wa klabu hiyo

Mkufunzi wa klabu ya Manchester United Jose Mourinho amesema kuwa hatosherehekea kama ''mtoto mwenye wazimu'' iwapo timu yake itafunnga dhidi ya Chelsea.

Mechi hiyo itakuwa mara ya pili kwa Mourinho kuelekea Stamford Bridge kama mkufunzi wa timu pinzani.

Alipata ushindi katika uwanja huo wakati akiwa mkufunzi wa Inter Milan mwaka 2010 ,kabla ya kujiunga tena kwa mara ya tatu na Bluez ambapo alishinda taji la tatu la ligi.

Image caption Jose Mourinho akisherehekea

''Nina ukomavu wa kudhibitia hisia'',alisema Mourinho.

''Iwapo timu yangu itafunga ,je nitasherehekea kama mtoto mwendawazimu? la hasha''.