Chelsea kukabiliana na Man United

Kocha wa Chelsea Antonio Conte Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kocha wa Chelsea Antonio Conte

Chelsea imesisitiza kuwa John Terry amepona jeraha la kifundo cha mguu lakini haijullikani iwapo ataanzishwa ,baada ya kuwekwa kama mchezaji wa ziada wikendi iliopita.

Willian na Oscar wamerudi katika mazoezi baada ya likizo lakini Cesc fabregas na Branislav Ivanovic wanaugua majeraha ya misuli.

Upande wa Manchester United beki Chris Smalling ambaye alilazimika kutoka nje wakati wa mechi dhidi ya Fenerbahce atakaguliwa jeraha alilopata.

Henrikh Mkhitaryan amepona jeraha lake la nyonga na huenda akachezeshwa.