Gor Mahia yailaza AFC Leopard

AFC Leopard dhidi ya Gor Mahia Haki miliki ya picha AF
Image caption AFC Leopard dhidi ya Gor Mahia

Gor Mhia wameimarisha matumaini yao ya kushinda taji la ligi ya Kenya baada ya kuwashinda wapinzani wao jadi AFC Leopard 2-0 katika uwanja wa Nyayo jijini Nairobi.

Ni mechi iliowavutia mashabiki wengi na siku ya jumapili haikuwa tofauti kwani masdhabiki wa Green army na wenzano wa Ingwe wakiujaza uwanja huo.

K'Ogalo walianza mechi hiyo wakijua kwamba matumaini yao ya kushinda taji hilo yatafifia iwapo hawatashinda,huku AFC Leopard nao wakibaini kwamba walihitaji tatu ili kuweza kupanda na kuorodheshwa katika nafasi nane bora.

Gor Mahia walipigwa jeki na kurudi kwa Collins gattuso Okoth ambaye alifanya mashambulio ya mapema baada ya George Odiambo wakuwachwa huru.

Meddie Kagere na Ennock Angwnda walifunga mabao hayo mawili.

Katika Mechi nyengine Tusker walitoka sare ya 1-1 dhidi ya Nairobi City Stars.