Mourinho na Man United waondoka darajani na kichapo

Chelsea 4-0 Man United
Image caption Chelsea 4-0 Man United

Jose Mourinho alifedheheshwa aliporudi katika uwanja wa Stamford Bridge baada ya timu yake ya zamani kuicharaza Manchester United.

The Blues ,ambao walimfuta kazi Jose Mourinho kwa mara ya pili mwaka uliopita waliongoza kunako sekunde ya 30 ya mchezo kuanza baada ya Pedro kupata mwanya katika safu ya ulinzi ya Man United.

Gary Cahill alifunga bao la pili katika kipindi cha pili baada ya United kuruhusu kona iliopigwa na Eden Hazard kudunda katika eneo la hatari la man United.

Image caption Chelsea ikikabiliana na Man United katika uwanja wa stamford Bridge

United hawakuonyesha ishara yoyote ya kukomboa mabao hayo ,na hivyobasi wakaongezwa bao la tatu na Eden hazard baada ya mchezaji huyo kupiga mkwaju wa umbalii wa maguu 15.

N'golo Kante aliimwaga safu ya ulinzi ya United na kufunga bao la nne na la mwisho na kuipatia ushindi Chelsea huku ikipanda hadi nafasi ya nne.

United watasalia katika nafasi ya 7 huku pengo kati yao na viongozi wa ligi likiongezeka na kufikia pointi tano.

Wakati huohuo viongozi wa Ligi Manchester City walitoka sare na Southampton katika uwanja wa Etihard.