Mrushaji mkuki bingwa Julius Yego apata ajali Kenya

Julius Yego Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mrushaji mkuki Julius Yego

Bingwa wa urushaji mkuki Afrika, Julius Yego, alinusurika baada ya gari lake kuhusika kwenya ajali ya barabarani mjini Eldoret, magharibi mwa Kenya.

Yego, ambaye alishinda fedha katika urushaji mkuki michezo ya Olimpiki Rio de Janeiro, Brazil, ameandika kwenye Facebook kwamba yupo katika hali nzuri.

"Mungu anaishi na ni mkuu! Niko salama watu wangu. Siamini kwamba niko hai. @mungu yupo! Nimo katika hali nzuri," Yego ameandika kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Picha za gari lake, ambalo limeharibiwa vibaya sehemu ya mbele, zimekuwa zikisambazwa sana mitandaoni Kenya.

Mashabiki wake wamekuwa wakimpa pole na kumtakia afueni ya haraka.

Haki miliki ya picha Julius Yego / Facebook

Yego alijifunza urushaji mkuki kwa kutumia video kwenye YouTube na kumfanya apewe jina 'Mwanariadha wa YouTube'.

Alishindwa ubingwa wa dunia wa urushaji mkuki wa IAAF mwaka 2015