Zamalek yasema "uchawi" uliwafanya kushindwa

Kocha mkuu Moamen wa Zamalek
Image caption Kocha mkuu Moamen wa Zamalek

Mwenyekiti wa Zamalek Mortada Mansour amelaumu "uchawi na bahati mbaya" kwa kushindwa kwa timu yake mikononi mwa timu ya Afrika Kusini ya Mamelodi Sundowns katika fainali ya ligi kuu barani Afrika.

"Kulikuwa na nafasi nyingi kwetu sisi katika mechi zote, lakini mpira ulikataa kutingiza nyavu" Mansour aliongeza, baada ya kushindwa mabao 3-1 kwa jumla ya mabao.

Pia aliunga mkono kwa kocha Moamen Soliman kusalia katika nafasi yake licha ya kupoteza.

"Tuna wakufunzi wazuri na sitawafuta kazi," amesema Mansour, mbaye aliwatumia wakufunzi sita mwaka huu.

"Kocha Moamen atasalia kama mkufunzi mkuu wa Zamalek, hadi mwisho wa msimu huu."