Wenger: Tuna fursa nzuri ya kushinda ligi

Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger
Image caption Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger

Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger amesema kuwa ana fursa nzuri ya kushinda ligi ya Uingereza msimu huu kwa mara ya kwanza tangu washinde taji hilo bila kushindwa mwaka 2004.

Akizungumza katika mkutano wa kila mwaka wa klabu hiyo,Wenger mwenye umri wa miaka 67,alisema kuwa mshindi wa taji la ligi kuu atakuwa na kati ya pointi 82 na 86 mwaka huu.

Alisema: Hii leo tuko katika nafasi nzuri zaidi ya kuwania taji la ligi ya Uingereza ikilinganishwa na miaka mitano au sita iliopita.

Ninaamini tuna timu nzuri katika ligi yenye ushindani mkubwa.

Arsenal ni wa pili katika jedwali la ligi,ikiwa ni mojwapo ya timu tatu zenye pointi 20 na wako katika nafasi ya pili kutokana na tofauti ya mabao.

Wenger anasema kuwa anafikiri kwamba anahitaji pointi 62 kutoka kwa mechi 29 zilizosalia kushinda taji .

Leicester ndio mabingwa wa taji hilo msimu uliopita.

''Baada ya mechi 9 ,tuna pointi 20,ikimaanisha kwamba ubingwa huo utaamuliwa na kati ya pointi 82 na 86'',alisema.