Jeraha latibua pigano la Klitschko dhidi ya Joshua

Klitschko kushoto na Anthony Joshua kulia
Image caption Klitschko kushoto na Anthony Joshua kulia

Bingwa wa ndondi anayemiliki taji la IBF katika uzani mzito duniani Anthony Joshua hatapigana tena na aliyekuwa bingwa katika uzani mzito duniani Wladmir Klitschko mwaka 2016 ,licha ya kwamba promota Eddie Hearn anatarajia pigano hilo baada ya msimu wa baridi.

Wawili hao walikaribia kuzichapa mnamo Disemba 10 lakini Klitschko akapata jeraha wakati wa mazoezi.

Taji la WBA pia halijasema iwapo litawaniwa au la.

''Huku akisubiri taji la WBA na huku Klitschko akiwa amejeruhiwa pigano hilo halikuweza kufanyika.Tupange pigano hili mwezi Machi ama Aprili'',alisema.

Hearn amesema kuwa Joshua atashindana huko mjini Manchester mnamo tarehe 10 lakini anatarajia tangazo rasmi kuhusu pigano hilo litakalofanyika 2017 baadaye wiki hii.