Liverpool, Arsenal na Tottenham kucheza EFL

Mechi kati ya Liverpool dhidi ya Tottenham Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mechi kati ya Liverpool dhidi ya Tottenham

Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger anatarajiwa kukibadilisha kikosi chake kitakachoshiriki katika raundi ya nne ya kombe la ligi dhidi ya Reading.

Vijana chipukizi Ainsley Maitland-Niles, Rob Holding, Jeff Reine-Adelaide na Chuba Akpom huenda wakashiriki pamoja na mshambuliaji Lucas Perez,huku Granit Xhaka akihudumia marufuku ya muda.

Reading wataelekea katika uwanja wa Emirates baada ya kumaliza msururu wa kupoteza mechi nne na ushindi dhidi ya Rotherham siku ya Jumamosi.

Wakati huohuo mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp anasema kuwa timu yake haijafikia kiwango cha asilimia 100 msimu huu licha ya kushinda mechi tisa.

Liverpool inakabiliana na Tottenham katika mechi nyengine ya siku ya Jumanne.

''Tunaweza kulinda lango letu,tunaweza kushambulia vizuri na tunaweza kutengeza nafasi nyingi'',alisema Klopp.