Aliyekuwa beki wa Brazil Carlos Alberto afariki

Carlos Alberto
Image caption Carlos Alberto

Aliyekuwa mchezaji mashuhuri wa timu ya Brazil Carlos Alberto ,ambaye alikuwa nahodha wa kikosi kilichoshinda kombe la dunia mwaka 1970 amefariki akiwa na umri wa mika 72.

Alifunga mojawapo ya mabao mazuri zaidi duniani katika historia ya kombe la dunia katika mechi ya fainali dhidi ya Italy mwaka 1970,baada ya kuwachenga mabeki na kufunga kupitia mkwaju mkali.

Beki wa kulia Alberto alichezeshwa mara 53 na Brazil na kushinda mataji ya nyumbani dhidi ya Fluminense na Santos ambapo alishiriki mara 400.

Alifariki mjini Rio de Janeiro kufuatia mshtuko wa moyo.