EFL: Alex Oxlade-Chamberlain awezesha Arsenal kulaza Reading

Oxlade-Chamberlain pia alifunga dhidi ya Nottingham Forest raundi iliyotangulia EFL Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Oxlade-Chamberlain pia alifunga dhidi ya Nottingham Forest raundi iliyotangulia EFL

Arsenal wameendeleza rekodi yao ya kutoshindwa hadi mechi 14 baada ya Alex Oxlade-Chamberlain kuwafungia mabao mawili na kuwawezesha kuondoka na ushindi dhidi ya Reading katika Kombe la EFL.

Kiungo huyo wa kati wa England alifunga bao la kwanza dakika ya 33.

Reading karibu wasawazishe baada ya mpira wakupinduliwa, wake Callum Harriott kutua juu ya lango lililokuwa linalindwa na Emiliano Martinez.

Arsenal walitawala mechi kipindi cha pili na Oxlade-Chamberlain akaongeza bao la pili dakika ya 78 na kuwawezesha kumaliza mechi ya 14 bila kushindwa.

Oxlade-Chamberlain, 23, alikuwa amesumbuka kupata nafasi kikosi cha kwanza timu ya Arsene Wenger mapema msimu huu.

Amecheza dakika 90 mechi mbili pekee, lakini kutokana na uchezaji wake mzuri karibuni, amempatia Wenger kila sababu ya kumpa nafasi kikosini.

Matokeo ya mechi za EFL

  • Arsenal 2-0 Reading
  • Bristol City 1-2 Hull
  • Leeds 2-2 Norwich
  • (Leeds United wakashinda 3-2 kupitia penalti)
  • Liverpool 2-1 Tottenham
  • Newcastle 6-0 Preston

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii