EFL: Sturridge asaidia Liverpool kulaza Tottenham Hotspur

Daniel Sturridge Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Daniel Sturridge sasa amefunga mabao tisa katika mechi nane za karibuni zaidi alizocheza Kombe la Ligi

Mshambuliaji Daniel Sturridge alifunga mabao mawili na kuwawezesha Liverpool kufika hatua ya robofainali Kombe la EFL kwa kulaza Tottenham 2-1 uwanjani Anfield.

Liverpool sasa wameenda mechi 10 bila kushindwa.

Sturridge aliwekwa benchi Jumamosi mechi waliyolaza West Brom na hakutumiwa.

Hata hivyo alihitaji dakika 10 pekee kufunga dhidi ya Spurs.

Jurgen Klopp alikuwa amebadilisha kikosi chache kizima kilichoanza mechi hiyo ya wikendi, Mauricio Pochettino naye akabadilisha wachezaji 10.

Spurs, walioanza na wachezaji wanane wa miaka 23 kwenda chini, walicheza vyema lakini walitatizika kushambulia hadi pale walipopata penalti iliyofungwa na Vincent Janssen baada ya nguvu mpya Erik Lamela kuchezewa visivyo eneo la hatari.

Sturridge aliongezea Liverpool bao la pili dakika ya 64.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Simon Mignolet akiokoa kombora la Vincent Janssen kipindi cha kwanza

Matokeo ya mechi za EFL

  • Arsenal 2-0 Reading
  • Bristol City 1-2 Hull
  • Leeds 2-2 Norwich
  • (Leeds United wakashinda 3-2 kupitia penalti)
  • Liverpool 2-1 Tottenham
  • Newcastle 6-0 Preston