Schweinsteiger arejea kikosi cha kwanza Man U

Schweinsteiger ameelezea kufurahishwa na kurejea kwake
Image caption Schweinsteiger ameelezea kufurahishwa na kurejea kwake

Mshindi wa kombe la dunia 2014, Bastian Schweinsteiger amerudi katika mazoezi na kikosi cha kwanza cha Manchester united.

Kiungo huyo mwenye miaka 32 amekuwa akifanya mazoezi na kikosi cha wachezaji wa chini ya umri wa miaka 23 tangu Jose Mourinho alipoteuliwa kuwa kocha msimu huu.

Nahodha huyo wa zamani wa Ujerumani kwa mara ya mwisho aliichezea Man U mwezi Machi wakati Louis van Gaal alipokuwa kocha wa mashetani hao wekundu.

Alisema mwezi August kuwa hana tatizo binafsi na Mourinho na Man U itakuwa klabu yake ya mwisho kucheza barani Ulaya.