London: Meya aamuru kufanyiwa uchunguzi uwanja wa West Ham

West Ham waliutumia uwanja huo kwa mara ya kwanza mwezi Agosti
Image caption West Ham waliutumia uwanja huo kwa mara ya kwanza mwezi Agosti

Meya wa jiji la London Sadiq Khan ameamuru kufanyika kwa uchunguzi juu ya ongezeko la gharama za Euro mil 50 wakati wa kuubadilisha uwanja wa West Ham.

Mwaka 2015, aliyekuwa meya wa jiji hilo Boris Johnson alisema kuwa kubadilishwa uwanja huo kutoka kuwa uwanja wa Olympic hadi kuwa uwanja wa mpira wa miguu ungegharimu £ milioni 272, kiasi ambacho sasa kimepanda hadi kufikia £ milioni 323.

Image caption Muonekano wa uwanja wa West Ham kwa ndani ambao majukwaa ya mashabiki yapo mbali na sehemu ya kuchezea

Paul Fletcher ambaye amehusika katika ujenzi wa viwanja zaidi ya 30, anasema ni lazima uwanja huo ujengwe upya kutokana na majukwaa ya mashabiki kuwa mbali sana na uwanja jambo ambalo halipendezi kwa mchezo wa mpira wa miguu.