UEFA: Man City yalipiza kisasi kwa Barcelona

Manchester City watafuzu hatua inayofuata kama wataifunga Borussia Monchengladbach Novemba 23
Image caption Manchester City watafuzu hatua inayofuata kama wataifunga Borussia Monchengladbach Novemba 23

Klabu bingwa barani ulaya iliendelea tena usiku wa kuamkia leo, ambapo kulikuwa na jumla ya michezo minane.

Manchester City wakiwa nyumbani walilipa kisasi dhidi ya Barcelona kwa kuichakaza magoli 3-1.

Washika bunduki wa london Arsenal waliendelea kudhihirisha ubabe wao mbele ya Ludogorets Razgrad ya Bulgaria kwa ushindi wa 3-2

Image caption Ozil ameelezea kufurahiswa na goli lake katika mtandao wa Twitter

Atletico Madrid wakiwa nyumbani waliibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya FC Rostov.

Bayern Munich ikaifunga PSV Eindhoven 2-1

Matokeo mengine

Basel 1-2 Paris Saint Germain

Besiktas 1-1 SSC Napoli

Benfica1-0 Dynamo Kyiv

Bourussia Moenchengladbach 1-1 Celtic

Manchester City 3-1 Barcelona