UEFA: Manchester City wapata ushindi wa kusisimua dhidi ya Barcelona

manchester City celebrate Haki miliki ya picha AP
Image caption Manchester City watafika hatua ya muondoano wakilaza Borussia Monchengladbach 23 Novemba

Manchester City wanahitaji kushinda mechi moja kufika hatua ya muondoano Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya baada ya kupata ushindi wa kusisimua dhidi ya miamba wa Uhispania Barcelona.

Mechi hiyo ilichezewa uwanja wa Etihad.

Lionel Messi alifunga bao lake la 90 ligi hiyo ya mabingwa baada ya kupokea pasi kutoka kwa Neymar na kuwaweka mbele Barca muda wa mapumziko ulipokuwa unakaribia.

Lakini mambo yalibadilika upesi kabla ya kipenga kupulizwa pale Sergi Roberto alipofanya kosa na Raheem Sterling akampa mpira Ilkay Gundogan ambaye alifunga kwa njia rahisi sana.

City, ambao walikuwa wanatafuta ushindi wao wa kwanza dhidi ya Barcelona katika mechi sita, walianza kudhihirisha ubabe wao kuanzia wakati huo na frikiki ya Kevin de Bruyne ilimuumbua kipa Marc-Andre ter Stegen dakika ya 51.

Mpira wa Andre Gomes uligonga mwamba huku Barcelona wakisaka bao la kusawazisha lakini City walijihakikishia ushindi wa kusisimua dhidi ya klabu ya zamani ya meneja wao Pep Guardiola zikiwa zimesalia dakika 16 pale De Bruyne alipompa pasi Jesus Navas naye akatoa krosi iliyomfikia mshambuliaji Sergio Aguero, kabla ya kumfikia Gundogan aliyefunga.

City watafuzu kwa hatua ya 16 bora iwapo watashinda Borussia Monchengladbach ugenini Novemba 23.

Gladbach walitoka sare na Celtic.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Gundogan alifunga mabao mawili na kukamilisha 96% kati ya pasi 28 alizotoa

Barcelona huenda walimkosa beki Gerard Pique na kigogo wa kati Andres Iniesta.

MATOKEO Kamili: Mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya

KUNDI A

Basel 1-2 Paris Saint Germain

Ludo Razgd 2-3 Arsenal

KUNDI B

Besiktas 1-1 Napoli

Benfica 1-0 Dynamo Kiev

KUNDI C

Bor Monchengladbach 1-1 Celtic

Manchester City 3-1 Barcelona

KUNDI D

Atletico Madrid 2-1 FC Rostov

PSV Eindhoven 1-2 Bayern Munich

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Manchester City walikuwa wameshinda mechi tano awali na Barcelona