UEFA: Arsenal watoka nyuma na kulaza Ludogorets Razgrad

Mesut Ozil Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mesut Ozil amefunga mabao manne mechi mbili za Ligi ya Klabu Bingwa alizocheza karibuni.

Mesut Ozil alifunga bao la dakika za mwisho na kuwawezesha Arsenal kutoka nyuma 2-0 na kulaza Ludogorets Razgrad ya Bulgaria na kuwafikisha hatua ya mondoano Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.

Ozil alionekana kutulia alipokimbia langoni, akampiga chenga kipa na mabeki wawili na kisha akatumbukiza mpira kimiani.

Awali, matumaini ya Arsenal kurudia ushindi wao mkubwa wa 6-0 mechi ya kwanza yalizimwa Jonathan Cafu alipowaweka Ludogorets mbele baada ya frikiki ya Wanderson.

Cafu alisaidia ufungaji wa pili alipomzidi ujanja Kieran Gibbs na kumpa mpira Claudiu Keseru aliyefunga na kuwashangaza Arsenal.

Granit Xhaka aliokoa jahazi upande wa Arsenal kwa kombora la kutoka hatua 15 kutoka kwa goli baada ya kupokea krosi kutoka Ozil na kufufua matumaini ya Arsenal kwa bao moja.

Olivier Giroud naye alifunga kwa kichwa kutoka kwa mpira uliotoka kwa Aaron Ramsey na kusawazisha.

Kipa wa Arsenal David Ospina alifanya kazi ya ziada kuokoa mpira mara mbili kutoka kwa Wanderson kabla ya Ozil kufunga.

Arsenal sasa wamefika hatua ya 16 bora na wameendeleza msururu wao wa kutoshindwa hadi mechi 15.

Haki miliki ya picha .

MATOKEO Kamili: Mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya

KUNDI A

Basel 1-2 Paris Saint Germain

Ludo Razgd 2-3 Arsenal

KUNDI B

Besiktas 1-1 Napoli

Benfica 1-0 Dynamo Kiev

KUNDI C

Bor Monchengladbach 1-1 Celtic

Manchester City 3-1 Barcelona

KUNDI D

Atletico Madrid 2-1 FC Rostov

PSV Eindhoven 1-2 Bayern Munich

Haki miliki ya picha Rex Features
Image caption "Mambo hayajaisha hadi yawe yameisha! Mwanzo mgumu lakini tumejikwamua vyema," Ozila aliandika kwenye Twitter baadaye