Guardiola: ushindi dhidi ya Barcelona ni mafanikio makubwa

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Guardiola anasema Man City walicheza kwa njia isiyo ya kawaida

Meneja wa Manchester City Pep Gurdiola anasema ushindi wa klabu hiyo wa mabao 3-1 dhidi ya Barcelona na ushinidi mkubwa kwa klabu yake.

Manchester City hawajawai kuwashinda Barcelona kwenye mechi tano ambazo zimepita na Guardiola anasema kuwa ni jambo lili zuri kusema kuwa kwa mara ya kwanza wamecheza na klabu bora zaidi duniani na kuwashinda.

"Tumeshindana na Barcelona, lakini kwa sasa tumefanya kwa njia tofauti. Tulicheza mipira mirefu kwa sababu hatuko tayari kucheza jinsi wanavyocheza." alisema Guardiola.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Guardiola alishinda kombe mara mbili akiwa na Barcelona mwaka 2009 na 2011

Ushindi wa Man City unaweka katika nafasi ya pili kwenye jedwali nyuma ya Barcelona ikiwa sasa inahitaji ushindi mmoja zaidi kutoka kwa mechi mbili zilizosalia kuweza kusonga mbele kwa kundi la timu 16 bora.

Guardiola ambaye alishinda kombe mara mbili akiwa Meneja wa Barcelona, alipata kipigo wakati Man City ilishindwa kwa mabao 4-0 uwanja wa Nou Camp mwezi uliopita.